globe Kiswahili Resource Center banner  
coursesbreakcontactsbreakmaterialsbreakweblinksbreakhome end
white  
 
Kiswahili Presentation Spring 2003
Mchezo huu umeandikwa na Abby Koch ( Rehema) na Emily Hall (Nyota) wanafunzi wa mwaka wa pili
May 7, 2003

Wahusika:
Nyota
Rehema
Mhudumu

Nyota: Jambo bibi. Mtu amekaa hapa?

Rehema: Sijambo! Karibu keti.

N: Asante bibi. Jina lako ni nani?

R: Jina langu ni Rehema. Na wewe je?

N: Jina langu ni Nyota. Unakipenda chakula hapa?

R: Ndiyo, ninakipenda sana. Mimi hupata kuku na ugali. Unakipenda chakula cha Afrika
ya Mashariki?

N: Ndiyo. Ninapenda chapati na mchuzi, lakini siwezi kupata chakula cha kigeni
nyumbani.

Mhudumu: Hamjambo!

R&N: Hatujambo!

M: Unataka kula nini?

N: Ninataka mchuzi na chapati.

R: Ninataka mchuzi na kuku.

N; Fanta ni bei gani?

M: Fanta ni shilingi ishirini.

N: Ninataka Fanta pia.

R: Ninataka chai.

M: Asanteni mabibi.

N: Mimi hula chakula cha Amerika….Nyama ya ng'ombe na viazi.

R: Kweli? Unatoka wapi?

N: Ninatoka mji mdogo katika jimbo la Kansas. Kuna Mkahawa mmoja hapo. Ninapenda hambaga na viazi vya kukaanga tu.

R: Pole sana! Mimi ninatoka jimbo la Kansas pia. Nilienda chuo kikuu cha Kansas, lakini niliondoka mwaka jana. Ninapenda mji mkubwa.

N: Kwa nini?

R: Kwasababu kuna watu wa namna nyingi. Miji mikubwa ni vituo vya utamaduni. Kuna maktaba na makumbusho mengi.

N: Ninajua. Ninaipenda miji mikubwa pia, lakini siwezi kuondoka jimbo la Kansas. Mama yangu ni mgonjwa na shangazi yangu ni mzee. Lazima niwaangalie.

R: Pole, pole sana! Una ndugu wa kukusaidia?

N: Nina ndugu watatu- wanawake wawili na mvulana mmoja, lakini hawanisaidii.

R: Kwa nini?

N: Kwasababu wanawake wameoa na wanakaa jimbo la Colorado, na mvulana ni mtoto tu. Ninamwangalia pia.

R: Kweli? Ndugu mdogo ana miaka mingapi?

N: Ana miaka kumi. Yeye anaenda shule ya chini. Ni mtoto mzuri sana, na mwenye akili.

R: Vizuri. Ndugu yangu anajua mama yenu ni mgonjwa?

N: Ndiyo. Mama yetu amekuwa mgonjwa kwa muda mrefu-miaka miwili.

R: Cha mno nini?

N: Ana kansa ya tumbo. Hawezi kula chakula, kwa hivyo hawezi kupata lishe na hana nguvu. Mara nyingine, anapata nafuu, lakini haponi. Lazima nimwendeshe ofisi ya daktari kila wiki.

R: Pole, pole sana! Mama yako ana maumivu?

N: Mara nyingine, lakini daktari anampiga sindano na anampa dawa vidonge.

R: Kwa nini ulimwondokea peke yake?

N: Usiwe na wasiwasi! Mama na ndugu yangu hawakai peke yao. Wanakaa katika nyumba ya jirani.

R: Ah, ninafahamu kwa nini ulienda mjini?

N: Mimi ni mwanafunzi, na sikuwa na darasa kwa wiki moja. Nilikuwa na nafasi kutembelea rafiki zangu hapa.

R: Vizuri! Ninafikiri unahitaji kupumzika.

N: Kweli. Ninapendezewa na safari yangu. Ninapenda mji huu. Umekaa hapa kwa muda gani?

R: Nimekaa hapa kwa miezi mitatu.

N: Unafanya nini?

R: Ninafanya kazi katika shule ya juu. Unafundisha lugha ya Kiswahili.

N: Vyema. Unapenda kufundisha?

R: Ninapenda kufundisha sana, lakini ni kazi shida.

N: Ninajua. Ni shida, hupati nyingi.

R: Ni kweli! Sina pesa nyingi, lakini ninajifurahia.

N: Vizuri. Umeoa au una wazazi hapa?

R: Hapana. Sijaoa, lakini haiduru. Wazazi wangu walikaa katika Kansas, na mji wa Lawrence.

N: Ulienda Lawrence kuwatembelea mara kwa mara?

R: Ndiyo. Ninakwenda Lawrence kila Krismasi, na mara nyingine katika majira ya joto.

N: Wewe huenda vipi? Kwa ndege?

R: Hapana. Ndege ni ghali sana, bora kwenda kwa motokaa. Safari hudumu masaa manane.

N: Ninajua ndege ni ghali. Nilienda hapa kwa basi.

R: Huna motokaa?

N: Hapana, sina motokaa. Nina pikipiki nyumbani. Siwezi kununua motokaa.

R: Kweli wewe ni mwanafunzi. Wanafunzi ni maskini.

N: Walimu pia.

R: Chakulu kiko hapa.

M: Mgependa Kitu Kingine?

R&N: Hapana, asante bibi.

R: Ndiyo. Sisi ni maskini. Unasoma nini katika chuo kikuu?

N: Ninasoma masomo ya Afrika ya Mashariki.

R: Masomo ya Afriki? Nitasafiri nchi ya Kenya mwezi ujao.

N: Vizuri! Kwa nini unaenda Afrika?

R: Nitakwenda kusoma katika chuo kikuu cha Kenyatta.

N: Kwa muda gani?

R: Kwa miezi miwili, katika Juni na Julai.

N: Utafanya nini tena katika Kenya?

R: Nitatembelea hifadhi za wanyama, kwenda pwani, kusafiri mji wa Mombasa, na kuona bonde la ufa na Mlima Kenya.

N: Utaona nini katika hifadhi ya wanyama?

R: Nitaona chui, twiga, tumbo, punda milia, na simba-na wengine. Nitasema na watu wa Kenya.

N: Utasafiri na wanafunzi wa chuo kikuu cha Kenyatta?

R: Ndiyo, wanafunzi wa chuo kikuu cha Kenyatta watasafiri pia.

N: Utavaa nini katiki Afrika ya Mashariki?

R; Nitavaa nguo zangu, lakini watu wa Kenya wanavaa mavazi mbalibali.

N: Kama gani?

R: Nguo kwa rangirangi, kimau, skati, malapa, na kanga, na buibui katika pwani na mji wa Mombasa.

N: Kwa nini watu wanavaa nguo mbalibali katika Mombasa.

R: Kwasababu watu wengi kutoka Mombasa ni Waislamu.

N: Kweli? Ninasoma dini ya Kiislamu katika chuo kikuu. Nguo ni rangi gani?

R: Nguo ni buluu, kahawia, urujuani, machungwa, waridi, na nyingine.

N: Utanunua vitu katika dukani katika sokoni?

R: Nitaweza kununua vitu vingi sokoni.

N: Utaweza kununua chakula, nguo, vitabu, stempu, na zawadi katika sokoni?

R: Ndiyo, nitaweza kununua vitu vingi, lakini sitnunua stempu.

N: Utaweza kununua stempu wapi?

R: Kununua stempu, lazima niende ofisi ya Posta. Nitaweza kupiga simu katika posta pia.

N: Posta iko wapi?

R: Lazima niulize dereva-Sijui.

N: Teksi ni ghali au rahisi katika Nairobi?

R: Teksi ni ghali sana, labda shilingi ishirini na tatu kwa maili moja!

N: Ghali sana! Utaweza kukodi motokaa?

R: Sipendi kukodi motokaa. Utasafiri kwa miguu au matatu.

N: Habari za hali ya hewa katika Afrika ya Mashariki?

R: Hali ya hewa ni nzuri, kwa kawaida digrii sitini na tano.

N: Utaenda kufarahia hapo. Natumai kwenda hapo siku moja.

R: Ninatumai utapata kusafiri Afrika pia.

N: Nina njaa.

R: Ni saa ngapi?

N: Ni saa moja jioni.

R: Nilifurahia mazungumzo yetu, lakini lazima niende nyumbani.

N: Mimi pia. Rafiki yangu ananingojea. Tunaenda karamu usiku, halafu tunaenda baa.
Ungependa kwenda pamoja na sisi?

R: Ndiyo, lakini siwezi. Lazima nitaamka mapema kesho. Ungetaka nikuendeshe nyumbani kwa rafiki yako?

N: Ndiyo, asante sana. Si mbali, lakini sipendi kwenda kwa miguu.

R: Rafiki anakaa wapi? Lazima unipe maelekezo.

N: Rafiki yangu anakaa, katika mtaa wa Washington karibu na ofisi ya askari.

R: Ah! Ninajua iko wapi. Twende.

N: Twende.

Mwisho




 
  African Studies Resource CenterbreakDept of African & African-American Studies end
this page mets accessibility guidelines
This website was originally developed with support from a U. S. Department of Education Title VI grant for "Enhancing Less Commonly Taught Languages and Cultures" (Award #P016A990036). This page was created by Jane Irungu with the assistance of Jonathan Perkins and Lewis Walton of the Ermal Garinger Academic Resource Center of the University of Kansas. Last modified May 3, 2004 .
KU Foreign Languages webpage