globe Kiswahili Resource Center banner  
coursesbreakcontactsbreakmaterialsbreakweblinksbreakhome end
white  
 

Mchezo wa kuigiza
Arusi ya Asha na Hamisi

Umeandikwa na wanafunzi wa mwaka wa pili
(A Play Written by Spring 2001 Second Year Students
[KIS 220] )

Wahusika:

  • Nyota............................ (Megan Collar)
  • Maua............................. (Mellanie Naaz)
  • Imani............................. (Noelle Johnson)
  • Hamisi........................... (Saju Ngalla)
  • Asha............................. ( Kathleen Korphage)

line

Sehemu ya kwanza
(sokoni)

Hamisi: Jambo ! Jambo msichana?

Asha: Jambo sana.

Hamisi: Ungependa kununua nini?

Asha: Ninataka kununua samaki.

Hamisi: Mkono wako ni mzuri sana.

Asha: Asante

Hamisi: Wewe una rafiki mvulana?

Asha: Tafadhali sitajibu swali.

Hamisi: Kwa nini?

Mama: Msichana unataka samaki? Tazama samaki zote ni nzuri na mpya

Asha: Asante. Jina lako ni nani?

Hamisi: Jina langu ni Hamisi Skywalker. Jina lako ni nani?

Asha: Jina langu ni Asha.

Mama: Msichana, unataka samaki au unataka mume?

Asha :( to Hamisi) Ninapenda jina lako Hamisi Skywalker.

Hamisi: Ninapenda nywele yako

Asha: Asante. Ninakupenda .

Hamisi: Ninajua

Asha: Bila shaka

Hamisi: Mwishowe tuposane?

Asha: Ndiyo, tuwe na arusi.

line

Sehemu ya pili
Nyumbani kwa akina Asha (at Asha's house)

(Wahusika) Mjomba wa Hamisi na Wazazi wa Asha.


Mjomba: Hodi!, Hodi!.

Wazazi: Karibu! Karibu ndani!

Mjomba: Hamjambo wazazi wa Asha. Mimi ni mjomba wa Hamisi. Najua ninafanana na Hamisi,
lakini mimi si Hamisi.

Mzazi: Nimefurahi kukutana nawe.

Mjomba: Ninakuja kwa ninyi kwa sababu mpwa wangu amemposa mtoto wenu. Ningetaka kutoa
posa

Wazazi: Tuna furaha mpwa wako anataka kuoa binti wetu. Yeye atakuwa mke mzuri kwa
hivyo tunatazamia mahari ghali.

Mjomba: Mambo ya mahari? Haya. Nimekuja ili tuzungumze habari hii na ninyi.

Wazazi: Mahari utatoa nini. Zawadi ni nini?

Mjomba: Hamisi atatoa mbuzi watatu kwa binti wenu.
(others gasp)

Wazazi: Do! hilo ni neno la kuchekesha? Binti wetu ni wa thamani zaidi ya mbuzi watatu.
Tumechukizwa sana.

Mjomba: Tafadhali mama, hamjachukizwa. Hamisi ni kijana na hana pesa nyingi. Mbuzi watatu
ni wengi.

Wazazi: Turuhusu binti wetu kuolewa na kijana maskini kama Hamisi?. Atatunza Asha na
watoto wao? Lakini kabla ya ujibu, karibu chai?

Mjomba: Ndiyo, asante sana. (tea is poured)
Hamisi ana mpango. Yeye atakwenda shuleni na atakuwa daktari wa kichwa. Halafu
atakuwa na pesa nyingi. Una sukari?

Wazazi: Ndiyo. (passes sugar)
Haya, lakini, je tunajua kama Hamisi atamaliza shule?

Mjomba: Atamaliza.

Wazazi: Haya, tutasema mahari sasa. Mbuzi watatu si wazuri. Tunataka mbuzi watatu,
ng'ombe wawili, na shilingi elfu nne.

Mjomba: Yale ni ghali sana sana. Mbuzi mmoja na ng'ombe mmoja.

Wazazi: Tunapenda sana binti wetu.

Mjomba: Itahitaji miaka kulipa! lakini atatoa ng'ombe mmoja na shilingi elfu mbili.

Wazazi: Vizuri sana. Karibu kwa jamaa yetu.

line

Sehemu ya tatu
Asha na marafiki:kudondoa mchele

Asha: Desturi za arusi ni nini katika Afrika ya Mashariki?

Imani: Tuna desturi nyingi hapa. Wanawake wanafanya matayarisho mengi kama kudondoa mchele na kupika biriani.

Maua: Ndiyo, tunafanya kazi nyingi kwa wiki mbili.

Nyota: Wakati wa arusi yangu katika Amerika…

Hamisi: Ninachukia kazi za arusi kwa sababu zina sherehe za arusi. Kwa sababu gani mama mzee alikuwa na arusi na mimi sina arusi?

Imani: Kwa sababu unalalamika sana.

Nyota: Kama Mimi nilikuwa nikisema…

Asha: Ninafurahi kwa sababu ninapenda desturi za arusi katika Afrika. Ninataka mnifundisha desturi zote za Afrika.

Nyota: Ninafikiri desturi za Afrika ni…

Imani: Vizuri sana! Tungependa kukufundisha desturi zetu!

Hamisi: Hapana, ninachukia desturi zo zote za arusi.

Maua: Sivyo, tunapenda kusaidia! Lakini, kwanza tukulishe.

Asha: Kwa nini?

Maua: Kwa sababu biarusi mnene ni biarusi mzuri.

Hamisi: Ninafikiri biarusi ye yote ni biarusi mbaya.

Asha: Katika Amerika, hatupendi biarusi mnene. Biarusi mwembamba ni mzuri. Biarusi katika Amerika hula kidogo kabla ya kuolewa.

Nyota: Ndiyo, biarusi mwembamba ni mzuri sana. Asha, wewe ni biarusi Mwamerika. Tutayarishe arusi ya Kiamerika. Unahitaji gauni nyeupe. Ni rahisi sana. Ninataka desturi za Amerika ndogo tu.

Asha: Haya, haya Mama. Tutakuwa na desturi nusu za Afrika na nusu za Amerika. Haya?

Nyota: Haya. Ni arusi yako. Usiharibu.

Hamisi: Nina sababu mpya kuchukia arusi. Kila mtu amekasirika sana.

Nyota: Nani amekasirika? Mimi sijakasirika. Maua, unakasirika?

Imani: Watu wote hawajakasirika. Lazima tusigombane.

Maua: Ndiyo! Na afadhali tudondoe mchele. Tupike biriani leo usiku.

Hamisi: Samahani, nitacheza mpira leo usiku.

Maua: Tafadhali, utatusaidia leo usiku. Ucheze kesho.

Hamisi: Lakini ninataka kucheza leo. Samahani.

Imani: Utaundondoa mchele sasa, Na leo usiku, utapika biriani.

Asha: Nina njaa sana.

Maua: Samahani Bi Asha! Nimesahau kukupa chakula. Tuna majadiliano mengi. Samahani. Unataka nini?

Asha: Ninataka matunda na mkate.

Maua: Haya. Tafadhali usubiri kidogo tu.

Imani: Usimame Maua. Hamisi, utupe chakula sasa.

Hamisi: Haya. Je, mama mzee, unataka chakula?

Nyota: Ndiyo, ninataka kuku wa kukangaa, na keki, na maziwa tu. Asante.

Hamisi: Nani anataka kusaidia kupata chakula?

Asha: Mimi ni biarusi, sitaki kusaidia.

Nyota: Sitaki kusaidia pia.

Imani /Maua: Mimi pia.

Hamisi: Je, Nani ni mvivu? Ninachukia arusi.

Asha: Mchele huu ni mchafu sana. Una mawe madogo mengi.

Maua: Ndiyo, lakini tutaundondoa vizuri sana na tutapika biriani bora pia.

Asha: Asante sana, rafiki. Je, tuna matayarisho mengine?

Imani: Ndiyo, tuna mengi kama kutengeneza mito na kununua gauni yako.

Maua: Ninapenda sana kutengeneza mito kwa sababu ninapenda dansi pia!

Nyota: Ninataka kununua gauni nyeupe sasa.

Asha: Ninataka kununua vitu vingine pia.

Imani: Haya, twende kununua vitu.

Hamisi: Walikwenda wapi? Nilikwenda kupika chakula na walikwenda kucheza. Ninataka kucheza pia, lakini hawaniachii kucheza. Ninachukia

line

Sehemu ya nne
karamu ya zawadi

(simu inalia…kriiii…kriiiii…..rafiki ya Asha anaita)
Asha: Hello! Hello!?

Maua: Hello, Asha. Huyo ni Maua. Jambo, habari gani, rafiki ?

Asha : Jambo Maua. Mimi ni mzuri sana. Utakuja nyumbani kwangu sasa hivi ?

Maua : Ndiyo. Nitakuwa hapo katika saa moja. Ninaita kuona kama unataka cho chote kutoka kwa duka?

Asha: Hapana, sihitaji cho chote, kwa sababu tuna chai na mkate mtamu hapa. Kuna chakula kingi; tutakunywa na kula. Hata hivyo asante.

Maua : Haya ndiyo. Je, unataharuki leo ?

Asha : Ndiyo, sana ! Ninataka zawadi! Zawadi nyingi!

Maua: Haya, nitakuona sasa hivi karibuni. Kwaheri !

Asha : Kwaheri, Maua !

(Baada ya saa moja )

Nyota: Hodi! Hodi!

Asha : Karibu, mama. Keti, tafadhali.

Nyota : Una siku njema, mtoto wangu ?

Asha : Ndiyo, mama. Ninafurahi leo kwa sababu nitapokea zawadi nyingi.

Nyota : Je, unafurahi utaozwa kesho, pia ?

Asha : (looking indifferent) Ndiyo.

(Nyota looks puzzled, and then there is another knock on the door)

Maua: Hodi, hodi!

Asha : Karibu, rafiki.

Nyota : Jambo, Maua? Nimefurahi uko hapa leo kuunga mkono karamu ya zawadi.

Maua : Asante. Asha, mkwe wangu yuko hapa ?

Asha : La, hajafika bado, lakini ninamtazamia sasa hivi.

Nyota : (to Asha) Unapenda mamake Hamisi ?

Asha : Ndiyo. Ninafikiri ni mzuri, lakini ana mtindo wa zamani. Mngoje; utaona.

(Hamisi's mother Imani knocks on the door)

Imani: Hodi, hodi!

Asha : Karibu, mama ! Tafadhali, njoo, keti.
Huyu ni mama yangu. Jina lake ni Nyota. Na, huyu ni rafiki yangu Maua.

Imani : Nimefurahi kukutana nanyi, sana !

Asha : Je, mnataka chai na mkate mtamu ?

Imani : Ndiyo Asha, tafadhali.

Nyota : Ndiyo Asha ninataka sukari na maziwa kwa chai yangu, pia?

Maua : Nitalete mkate mtamu na chai kwa kila mtu.

Nyota : Uko tayari kufungua zawadi zako, Asha ?

Asha : Do ! Niko tayari, sana !

Maua: Hapa ni zawadi zangu, Asha.

Asha : Asante rafiki, Ninazipenda ! Mimi nina hakika Hamisi atazipenda, pia.

Nyota : Ninafikiri atazipenda.

(Imani looks shocked!)

Nyota: Hizi ni zawadi zangu, Asha.

Asha : (disappointed) Nzuri sana mama. Ninazipenda.

Maua: (also disappointed) Ndiyo, nzuri, nzuri sana.

Imani: Ninazipenda! Sasa nitakupa zawadi zangu. (She hands Asha cooking utensils)

Asha: (hesitantly) Umm…Asante mama.

Imani: Nafikiri umezipenda ! Upike kwa wingi . Ni madaraka kuwa mke wa Hamisi. Uzae watoto wengi, pia. Kumi au kumi na wa tano, pengine. Ninataka wajukuu wengi !

Asha: (in shock) Samahani, mama Imani, lakini ninataka kwenda Chuo Kikuu na kuwa na maisha na kazi.

Imani: Unafikiri vibaya, mtoto! Madaraka ya Hamisi kuwa na mke mzuri, kwa hivyo ufanye kazi nyumbani!

Nyota : Mama Imani, hana haki. Ni hiari ya Asha.

Imani : Hupatani na mimi, mama Nyota ?

Nyota : Haidhuru rai yao. Asha anaruhusiwa kukaa kwa furahi. Tujifunze kuwasaidia Hamisi na Asha kwa sababu wao ni wazuri.

Maua : Haya napatana !

Imani : Kama Asha na Hamisi wanafurahi, mimi pia.

Asha : Vizuri sana. Twende baa kwa karamu ya wasichana, sasa !

Wote : Haya!

(Katika dansi ya karamu…)

Nyota: Mahali hapa ni pakubwa pana kishindo.

Maua: Tutakuwa na wakati wazuri. Utauona, Mama!

Imani: Tazama. Mvulana yule anacheza kama kuku.

Asha: Ndiyo, ana kichaa!

(everyone laughs)

Hamisi: Hamjambo wanawake warembo.

Asha: Jambo, kuku

Hamisi: Je, unasema nini?

Maua: Anasema "jambo, ndugu"

Hamisi: Mnanichezea mtaona!

Nyota: (to Asha) Binti yangu, ununue bia, tafadhali.

Maua: Asha na mimi tunawaletea bia.

Imani: Nzuri, asante watoto.

(later…the mothers become drunk)

Nyota: (to Hamisi) Kuku! Njoo hapa tucheze!

Hamisi: Bei ni dola kumi.

Imani: Nitakupa dola nne.

Hamisi: Haya, lakini hawanigusi au bei itakuwa dola ishirini!

(Hamisi's dance is over and the ladies are laughing and being drunk, especially the mothers)

Nyota na Imani: Asante, kuku!

Door Man: Haya, wanawake. Mwende, sasa, Ninyi walevi

Asha: Ninaona haya sana.

Imani: Nyota, unaangusha bia yangu! Hapa, unywe bia yangu.

Door Man: tunaleta wanawake.

Asha: Samahani, bwana. Wanatuzui kushangilia! Wanasumbua sherehe!

Door Man: Mwondoke, sasa!

line

Sehemu ya tano
sherehe ya kuunganisha bi na bwana arusi

Muhubiri: Asha na Hamisi wameadikiana nadhiri wenyewe. Kuunga mkono nadhiri tafadhali
sema tena. Asha…utasema nadhiri kwa Hamisi. Mimi Asha

Asha: Mimi Asha (Asha anamtazama Hamisi)

Mhubiri: Ninakupenda Hamisi kwa sababu wewe mtu mrembo…

Asha: Ninakupenda ...........

Hamisi: (gazing at the beautiful bride) Mimi Hamisi..

Mhubiri: ninamchukua Asha kama mke wangu, nitamwekea tayari pesa na wanyama, halafu nitampa moyo wangu kwa maisha.

Hamisi: ninamchukua............................... kwa maisha.

Mhubiri: Haya, vizuri sana. Sasa, nani anapete?
(Groomsman and Maid of Honor- together they get out the rings) Sisi tuna pete
hapa .

Mhubiri: Halafu, mtasema tena… Hamisi… kwa pete hii ninakuoa…

Hamisi: Asha, kwa pete hii ninakuoa…

Mhubiri: Hamisi, unachukua msichana huyu kuwa mke wako katika ugonjwa na
afya; mpaka kifo?

Hamisi: Ndiyo! (he puts the ring on her finger and blushes)

Mhubiri: Haya, Asha…sema tena…kwa pete hii ninakuoa…

Asha: Hamisi, kwa pete hii ninakuoa…

Mhubiri: Je, Asha, unachukua kijana huyu kuwa mme wako katika ugonjwa na
afya; mpaka kifo?
Asha: Ohhh, Ndiyo, ndiyo! (she puts the ring on his finger and they hug, both
smiling)

Mhubiri: Sasa, ninyi mtaanza kuwa mke na mme!!! hoyee!(the bystanders cheer)
Hamisi, unaweza kubusu mke sasa.


MWISHO



 
  African Studies Resource CenterbreakDept of African & African-American Studies end
this page mets accessibility guidelines
This website was originally developed with support from a U. S. Department of Education Title VI grant for "Enhancing Less Commonly Taught Languages and Cultures" (Award #P016A990036). This page was created by Jane Irungu with the assistance of Jonathan Perkins and Lewis Walton of the Ermal Garinger Academic Resource Center of the University of Kansas. Last modified May 3, 2004 .
KU Foreign Languages webpage