globe Kiswahili Resource Center banner  
coursesbreakcontactsbreakmaterialsbreakweblinksbreakhome end
white  
 

Safari ya Tanzania

Insha imeandikwa na Sara Smiley

Machi 2004

Juni hii, nitasafiri nchi ya Tanzania , mji wa Arusha. Nitasoma Kiswahili. Nitaenda kwa chuo kikuu cha Georgia na Mwalimu Moshi. Nitaenda pamoja na wanafunzi kumi na wanne. Darasa linaitwa “Group Project Abroad” na linalipwa na serikali ya Amerika. Serikali itanilipia vyakula, vyumba vya kulala, na vyeti vya ndege. Sasa, nimesoma katika chuo kikuu cha Kansas . Nimesoma jiografia ya Afrika Mashariki. Kwa hivyo, nimesoma Kiswahili kwa miaka miwili. Madarasa yamenitayarisha kwa safari. Sijawahi kwenda Afrika. Ninafurahi kwa safari

.

Kujitayarisha kwa safari, nimesema na Mwalimu Irungu, Mwalimu Myers, na mwenzangu. Yeye anatoka Tanzania na jina lake ni Mohamed. Nimesoma vitabu vya Kiswahili, nimesikiliza kanda ya sauti kwa Kiswahili, na nimeandika maandishi kwa Kiswahili.

Nitasafiri Tanzania tarehe ishirini. Nitaendesha kwa jimbo la Kentucky na nitakaa na wazazi wangu. Nitasafiri mwezi wa Mei, tarehe ishirini na sita. Halafu, nitaenda jimbo la Michigan , mji wa Detroit . Nitaenda kwa ndege. Katika Detroit, nitakutana na wanafunzi wengine. Sikutani na wanafunzi kwa sababu wanasoma ktika vyuo vikuu tofauti kama Indiana , Boston , Michigan State, na kadhalika. Tutaenda Tanzania pamoja. Tutapita mji wa Amsterdam . Tutafika Arusha tarehe ishirini na moja.

Tukifika Arusha, tutaenda kwa bweni. Tutakaa kwa “ Training Center .” Center ni shule. Ina vyumba vya madarasa, vyumba vya kulala, jikoni, chumba cha kula, chumba cha starehe, na uwanja wa michezo. Center ina wanafunzi wengi. Wanafunzi wanatoka Ulaya, Amerika, na Afrika. Wanafunzi ni wanafanya kazi, si watoto. Center inafundisha Kiswahili na Kiingereza.

Tutasoma Kiswahili. Tutakuwa na madarasa Jumatatu hadi Ijumaa. Tutasoma kwa masaa sita kila siku. Kwa wikiendi, tutasafiri huko Tanzania . Tutasafiri Bagamoyo,

Unguja,

Dar es Salaam , na Moshi. Tutaona kijiji cha Masaai, shamba la kahawa, na chuo kikuu cha Dar es Salaam . Tutakutana na watu wengi: walimu, wanafunzi, na watu wa serikali. Wikiendi ya nne, tutakaa kwa “host families.” Kila mwanafunzi atakuwa na jamii. Nitatumai jamii yangu wana watoto. Nitajifundisha Kiswahili wakati nitasema na watoto. Nitajifundisha Kiswahili cha miji.

Ningependa kwenda nchi ya Kenya na nchi ya Uganda . Kwa shahada ya pili, nilisoma juu ya Uganda . Nilisoma jiografia ya deni. Nilisema na watu wazuri na ningependa kukutana nao. Safari nyingine, nitaenda Uganda .

Kwa shahada ya tatu, nitasoma Kenya. Nitasoma jiografia ya fasihi. Nitasoma vitabu vya Ngugi wa Thiong'o

 

kama Petals of Blood , Matigari , na Devil on the Cross . Nitasoma jiografia ya miji, vijiji, na serikali. Nitapenda kufanya utafiti kwa Kenya .

Safari yangu itakuwa nzuri sana lakini maisha yangu yatakuwa mbalimbali. Nitakula vyakula vipya. Sasa, mimi ni mla mboga. Katika Tanzania , nitakula nyama. Wakati nitakaa na jamaa wangu, nitakula vyakula vya Tanzania : nyama ya ng'ombe, mbuzi, na samaki. Vyakula hivi vitakuwa nzuri. Pia, nitataka kula vyakula vingine: maandazi, chapati, ugali, na irio.

Nimetayarisha mwili wangu. Niliona daktari. Tulisema juu ya dawa. Alinipiga sindano kwa homa ya manjano, pepopunda, homa ya matumbo, na ugonjwa wa manjano. Daktari alinipa dawa kwa homa ya malaria. Kwa usiku, nitavaa suruali. Nitatumia mdudu ya kuchukiza. Nitalala chini ya chandarua. Kwa Tanzania, siwezi kunywa maji. Nitanunua maji ya chupa. Siwezi kula ngozi ya matunda na mboga. Ngozi yangu ni nyeupe sana . Kwa hivyo, sioti jua. Ninajipaka mafuta ya kuota jua. Kama nitakuwa mgonjwa, nitaona daktari. Tanzania ina daktari kama Amerika.

Nitabeba vitu vingi. Nitabeba nguo, vitabu, madaftari, kalamu, na mahitaji ya binafsi. Nitabeba nguo ya pamba. Nimenunua sketi na nguo za wanawake. Ninataka kununua kanga sana pia. Sitavaa suruali ndefu au suruali fupi. Nitabeba kitabu cha Kiswahili. Nitanunua kitabu cha darasa. Jina chake ni Colloquial Swahili . Nitabeba vitabu kusoma kwa furaha. Ninapenda Jurassic Park na vitabu vya mafumbo. Nitabeba kamusi ya Kiswahili pia. Nitabeba sabuni ya mwili, sabuni ya uso, shampuu, kiondoa harafu, na losheni. Vitu vingine nitanunua huko Tanzania .

Mwalimu Moshi, aliniambia kuleta kalamu na kalumu ya rangi kwa watoto. Nitaleta vitabu kupa maktaba ya chuo kikuu. Kwa jamaa wangu, nitabeba zawadi. Kwa mama, nitampa herini. Kwa baba, nitampa tai. Kwa dada au kaka, nitampa mpira wa soka au kanda ya sauti.

Katika Tanzania, nitanunua zawadi. Kwa mama, nitamnunua kanga, sanaa, na chombo cha muziki. Yeye ni mwalimu na anapenda kuona wanafunzi vitu vya Afrika. Kwa baba, nitamnunua pombe, kanzu, na nguo. Anapenda kuvaa nguo za mahali mbalimbali. Anapenda kuambia watu kwa dada wake. Kwa dada, sitamnunua vitu. Nitapiga picha sana na nitampa picha. Kwa rafiki, nitawanunua vitabu na kanga. Kwa Mwalimu Myers, nitamnunua muziki. Anataka muziki kwa utafiti wake. Kwa Mwalimu Irungu, nitamnunua magazeti na vitabu vya watoto.

Ninaogopa kwa vitu vichache. Ninaogopa homa ya malaria. Ninaogopa kwamba Kiswahili changu ni kibaya. Nitataka kusema na watu. Kama Kiswahili changu ni kibaya, siwezi kufahamu watu. Ninaogopa lakini safari yangu itakuwa nzuri sana . Wakati Tanzania , sitaogopa. Nitakuwa na furaha.

Wakati nitarudi, Kiswahili changu kitakuwa kizuri kuliko sasa. Nitatumai kwamba mimi ni fasaha. Ningependa kusoma vitabu vya Kiswahili. Nitapenda kufahamu vitabu. Sitatumia kamusi sana .

Ninapenda Kiswahili sana . Ninapenda lugha, watu, na utamaduni. Ninatumai kwamba ninapenda maisha ya Waswahili pia. Maisha itakuwa tofauti lakini ninajitayarisha. Ninataka kwenda Tanzania leo!



 
  African Studies Resource CenterbreakDept of African & African-American Studies end
this page mets accessibility guidelines
This website was originally developed with support from a U. S. Department of Education Title VI grant for "Enhancing Less Commonly Taught Languages and Cultures" (Award #P016A990036). This page was created by Jane Irungu with the assistance of Jonathan Perkins and Lewis Walton of the Ermal Garinger Academic Resource Center of the University of Kansas. Last modified January 21, 2005 .
KU Foreign Languages webpage