globe Kiswahili Resource Center banner  
coursesbreakcontactsbreakmaterialsbreakweblinksbreakhome end
white  
 

Majimbo ya Kentucky na Kansas

Insha ambayo iliandikwa na Sarah Smiley, mwanafunzi wa mwaka wa tatu

Novemba 2004

Ninatoka jimbo la Kentucky lakini sasa ninakaa jimbo la Kansas . Ninafikiri kwamba nina nyumba mbili: Kansas na Kentucky . Nitazungumza kuhusu majimbo mawili haya, hasa historia, maelezo, na burudani zao.

Jimbo la Kentucky

Nilizaliwa jimbo la Kentucky , mji wa Louisville tarehe 27, mwezi wa Julai, mwaka 1978. Familia yangu ilihamia mji wa Lexington mwaka 1987. Nilipokuwa mtoto mdogo, mimi na familia yangu tulisafiri pengi katika jimbo. Baba yangu, alifanya kazi katika serikali ya Kentucky kwa hivyo tulikaa katika mbuga za jimbo. Tuliona mahali pa historia kama Ngome ya Boonesboro, Ngome ya Knox (mahali ambapo dhahabu zinakaa), na nyumba ambayo inaitwa “My Old Kentucky Home”. Nyumba hii ina wimbo ambao uliandikwa kuuhusu. Mahali nilipopenda palikuwa mbuga ya wanyama ya Louisville . Nilienda mahali hapa kila wikiendi nilipoishi mji huu. Nilipenda tai ambaye hakuwa na nywele (au ‘Bald Eagle'), ndege wa taifa Marekani.

Kentucky ilijiunga na nchi ya Marekani mwaka 1792. Mji mkuu wa Kentucky ni Frankfort lakini watu wengi wanafikiri mji mkuu ni Louisville kwa sababu Louisville ni mji mkubwa kuliko Frankfort . Baba yangu anapenda kutani kwa masihara haya: “Unavyosema jina la mji mkuu: Louie-ville au Loo-a-vul?” Mtu anapojibu, baba anasema: “Hapana. Unavyosema Frankfort”. Anafikiri masihara yake ni mazuri lakini mama yangu na mimi tunajua masihara ni mabaya sana .

Vita vya Marekani vilikuwa muhimu sana kwa Kentucky . Familia nyingine ambayo ilikaa Kentucky kumiliki watumwa na familia nyingine ambayo ilikaa Kentucky haikumiliki watumwa. Vita vilihusu watumwa na kama watu waliweza kumiliki watu wengine. Vita vilipomalizika, serikali ilisema “Ilikuwa haramu kuwa na watumwa.” Leo, watu wanaweza kuona nyua ambayo ilijengwa na watumwa.

Watu ambao wanafanya kazi katika Kentucky wanafanya kazi mbalimbali. Watu wengine wanafanya kazi kwa kampuni, shule, serikali, na mahali pengine. Watu wengine ni wakulima. Wanapanda mimea tofauti lakini Kentucky ni muhimu kwa tumbako. Watu wegine wanafuga farasi. Farasi hizi ni ghali sana na wanakimbia haraka. Shindano kuu la farasi linaitwa “Kentucky Derby”na watu wengi wanakuja kuona shindano.

Wanawake wanavaa kofia kubwa na wanamume wanavaa suti. Nilienda shindano mara moja tu kwa sababu tiketi ni ghali sana . Pia, nilienda mashamba ya farasi. Nyumba za farasi ni nzuri na kubwa kuliko nyumba yangu. Watu wengine wanafanya wiski. Wiski ni kinwaji na aina muhumu inaitwa “Jim Beam.” Sipendi kunywa wiski.

Kuna vitu burudani kuhusu Kentucky . Sikukuu ya mama ilianza hapa mwaka 1887. Kentucky ni nyumba kwa pango mrefu katika dunia. Linaitwa “ Mammoth Cave .” Taa ya umeme kwanza ilionekana katika Kentucky mwaka 1883. Thomas Edison alibuni taa hiyo na alileta taa hapa.

 

Jimbo la Kansas

Nilihama jimbo la Kansas mwaka 2001 nilipoanza kusoma katika Chuo Kikuu cha Kansas . Kabla ya kutembelea Chuo Kikuu cha Kansas , sijawahi kuvuka Mto wa Mississippi ! Nilifikiri kwamba Kansas ilikuwa usawa kama gole au ukarasa lakini nilistaajabu. Mji wa Lawrence una vilima vingi. Hata hivyo, Lawrence ni tofauti kuliko miji ya Kansas mingine. Watu ambao wanaishi Lawrence ni ‘Democrats'. Wiki ijao, watu wengi watapiga kura kwa John Kerry.

Takriban maili hamsini magharibi wa Lawrence, hakuna vilima. Badala yake, kuna mashamba mengi. Wakulima ambao wanaishi sehemu hii, wanapanda ngano sana . Jimbo la Kansas linaitwa “Kikapu cha Mkate cha Dunia.” Kila mwaka, wakulima hawa wanapanda ngano kutosha kumpa kila mtu mikate sita!

Jimbo la Kansas lilikuwa na historia kwa Vita vya Marekani pia. Kansas ilikuwa “Jimbo la Huru.” Kwa hiyo, watu hawakukuwa na watumwa. Missouri ilikuwa “Jimbo la Watumwa.” Kwa hivyo, watu ambao walitoka Kansas walipigana na watu ambao walitoka Missouri . Mwanaume ambaye aliitwa Quantrell aliongoza safari kwa Kansas . Yeye alianza moto kwa Lawrence kwamba uliwaka majumba mengi ambayo yako katika mtaa wa Massachusetts .

Kansas iliunga nchi ya Marekani mwaka 1861. Mji mkuu ni Topeka . Topeka ni magharibi mwa Lawrence . Nilienda Topeka mara moja nilipotazama mpira wa kikapu. Mume wa rafiki yangu alikuwa kocha katika shule ya msingi. Siku moja, ningependa kuona jumba la serikali. Nilisoma kuhusu sanamu ambayo iko juu ya jumba. Sanamu inaona methali ya jimbo. Methali inasema “Enda nyota kupita Ugumu.”

Kuna vitu burudani kuhusu Kansas . Kansas ilikuwa mahali pa kuzaliwa pa wanawake muhudimu. Meya wa kwanza mwanamke alifanya kazi katika mji wa Argonia. Mchezaji wa kwanza Mmarekani-Mwaafrika ambaye alishinda ‘Oscar' alitoka Kansas . Aliingiza mchezo katika “Enda kwa Upepo.”

 

Maelezo Kuhusu Majimbo

 

 

Kentucky

Kansas

Numba za Watu

4,117,827

2,688,418

Eneo

39,728 maili ²

81,815 maili ²

Jina la Utani

Bluegrass State

Sunflower State

Maua

Goldenrod

Sunflower

Ndege

Cardinal

Western Meadowlark

Nyama

Thouroughbred Horse

American Buffalo

Mti

Tulip Tree

Cottonwood

Wimbo

My Old Kentucky Home

Home on the Range

Vyuo Vikuu

32

27

 

 

Ninapenda Kentucky na Kansas sawasawa. Zote ni nyumba zangu. Ninapotembelea wazazi wangu, ninatamani Kansas na mara kwa mara ninatamani Kentucky . Siku moja, nitahama jimbo lingine na jimbo hili litakuwa nyumbani pia.

 


 
  African Studies Resource CenterbreakDept of African & African-American Studies end
this page mets accessibility guidelines
This website was originally developed with support from a U. S. Department of Education Title VI grant for "Enhancing Less Commonly Taught Languages and Cultures" (Award #P016A990036). This page was created by Jane Irungu with the assistance of Jonathan Perkins and Lewis Walton of the Ermal Garinger Academic Resource Center of the University of Kansas. Last modified January 19, 2005 .
KU Foreign Languages webpage