Afrika ya Mashariki Leo

 

Juma Shmalberg,

Mwanafunzi wa Kiswahili, mwaka wa pili

Tarehe Saba, Mwezi wa Novemba, 2002

 

Katika Afrika ya Mashariki leo, kuna habari nyingi. Kwa mfano, raia wa Kenya watapiga kura katika mwezi wa Desemba, Rais Moi wa Kenya amevunja kamati ya katiba, kuna mapigano Uganda ya Kaskazini, viongozi wa Afrika ya Mashariki wanajadili desturi na dini, na watu wangependa kuona watalii zaidi.

Kwanza na muhimu ni uchaguzi mkuu, nchi ya Kenya.Rais Moi hawezi kuchaguliwa kwa sababu ya katiba ambayo imemzuia kwa kuwa mgombezi uchaguzi. Lakini Rais Moi angependa kuona Uhuru Kenyatta, mtoto wa kiume wa rais kwanza Kenyatta, kuchaguliwa kwa ofisi kuu ya nchi. Sasa chama kikubwa, jina ni KANU, kitahitaji kushinda chama cha upinzani, chama cha Rainbow. Viongozi wa chama cha Rainbow wanaamini mgombezi wao, makamu wa rais wa awali wa Moi, Bwana Mwai Kibaki, ataweza kumshinda Kenyatta. Uchaguzi mkuu utakuwa mwezi wa Desemba, tarehe ishirini na saba, mwaka huu na utagharimu dola milioni hamsini na nane. Uchaguzi si swali tu la rais na baada ya hapo, ni swali kubwa la kama demokrasi kweli inaweza kuanza katika Kenya.

Kwa sababu Rais Moi alihitaji kuvunja bunge kwa uchaguzi, huku kunamaanisha kamati ya katiba ilivunjwa pia. Mwalimu Ghai, ambaye ni mwenyekiti wa kamati, amesema yeye anafikiri bunge tu inaweza kuivunja kamati hii. Hata hivyo, watu wanaogopa rais mpya atahitaji kuanza kamati mpya kwa katiba. Kama Uhuru Kenyatta atachaguliwa, huku lazima kuwe shida, lakini Kibaki amesema yeye anataka katiba mpya na atafanya kazi kwa huku. Jambo hili lilisabibisha utumizi wa dola milioni tano, na watu wengi wameliunga mkono. Rais Moi alisema chama cha upinzani tu kiliitaka kwa sababu katiba mpya itawapa uwezo mkubwa. Kwa sasa, raia wa Kenya wanaweza kungojea tu kwa mabadiliko.


Pia katika nchi ya Kenya, kumekuwa majadiliano ya desturi ya arusi na mahari. Vijana wa makabila ya Turkana na Pokot, upande wa kaskazini katika nchi ya Kenya, wamesema huhitaji kupigana na kuziiba ng'ombe kwa mahari ya desturi. Viongozi katika kaskazini wametafutia serikali kuu kwa msaada. Siku mbili baada ya hii, Sheikh Ali Shee, kiongozi wa Waislamu wa Kenya, alisema lazima kusiwe na mahari kwa sababu gharama hizi huzungukia wanawake "watumishi na watumwa."


Katika sehemu ya kaskazini ya Uganda, kuna mapigano kati ya serikali ya Uganda na waasi wa Jeshi la Upinzani wa Mungu, au kwa Kiingereza, the Lord's Resistance Army. Chama cha haki za binadamu katika Amerika kimesema waasi na serikali wametumiwa vibaya kwa miezi iliyopita michache. Ni kweli zaidi ya watu nusu ya milioni wamekaa vijiji vya maskini kwa sababu mapigano katika sehemu hii ya nchi. Katika mwezi wa Septemba, mwaka wa elfu mbili na mbili, mia tano na hamsini elfu waliondoka na hawana vyakula wala shamba. Pia, kuna Wasudan elfu ishirini na wanne ambao hawana nyumba katika Uganda.

Wizara wa Mambo ya Nje wa Marekani imesema kuna fadhaa kati ya Wakristo na Waislamu katika nchi ya Tanzania. Taarifa ya mwaka inasema kuna maoni ya dhidi ya Wakristo masehemu ya Dar es Salaam, Morogoro, na Zanzibar. Asilimia ya sehemu ya Waislamu ni thelathini au arobanini. Serikali ya Amerika ilisema kuna uhusiano wa uhuru wa dini katika nchi ya Tanzania.


Ijapo kuna vitu vibaya vichache katika habari ya Afrika ya Mashariki leo, kuna watu wazuri, vitu vizuri kufanya katika nchi, na bei nzuri ya bidhaa. Kwa hoja hii, viongozi wa Afrika ya Mashariki wangependa kupendeza watalii zaidi. Tarehe ishirini na tisa, watu wa shughuli ya utalii walijadili vipi watalii zaidi wataweza kuenda Afrika ya Mashariki. Bwana James Babihinguza, meneja wa Kamati ya Utalii ya Uganda au Uganda Tourist Board (UTB), alisema, "Kuna faida ya matumzi wa kusifu wa mali asili, kwa mfano, Kenya ina bahari na pwani, Uganda ina sokwe na spishi za ndege na Tanzania ni yenye sifa kwa mali ya mwitu kama wanyama."

 

Picha zote za BBC News Online